Usikose Hizi Hapa

VIDEO-;SPURS YAKIONA CHA MOTO KWA CHELSEA NYUMBANI KWAO

Hatimaye Chelsea imepata ushindi wa kwanza ugenini kwa kuichapa Tottenham Hostpurs magoli 2-1 baada ya wiki iliyopita kuambulia kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Burnley katika uwanja mpya wa Tottenham uitwao Wembley.

Shukrani kwa mchezaji wa Chelsea Marcos Alonso aliyeng'ara katika mechi hiyo akifunga mabao mawili na kuwa mchezaji wa mechi 'MAN OF THE MATCH'

Marcos Alonso alianza kufunga goli dakika ya 24 kupitia free kick baada ya David Luiz kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Tottenham Delle Ali na refa kuamua iwe foul.

Baadaye dakika ya 82 Michy Batshuay aliigharimu Chelsea kwa kujifunga mwenyewe kwa kichwa baada ya kupigwa free kick na Christian Ericksen wa Tottenham na kisha ubao kusomeka 1-1.

Dakika ya 88 Marcos Alonso akawainua mashabiki tena katika dimba la Wembley kwa shuti lililombabatiza kipa Hugo Lloris hatimaye kuingia wavuni na Chelsea kushinda mchezo huo wa ligi kuu ya Uingereza EPL.

Hata hivyo Spurs ilionyesha kiwango cha juu na kukosa nafasi nyingi walizotengeneza wakati Chelsea walizitumia vema nafasi chache walizotengeneza na kushinda mchezo huo.

Mechi hiyo ilikuwa na kadi nyingi za njano ambapo wachezaji waliopewa ni Antonio Reudiger (Chelsea dk 30), Erick Dier (Tottenham dk 31), David Luiz (Chelsea dk 38), Jan Vertonhen (Chelsea dk 51), wengine ni Toby Alderweireld (Tottenham dk 83), Marcos Alonso (Chelsea dk 87) na Hary Kane (Tottenham dk 88)

TAZAMA MECHI KATI YA SPURS NA CHELSEA KAMA ULIPITWA>>>>>> Mchezo mwingine wa ligi kuu Uingereza uliopigwa leo ni kati ya Huddersfield dhidi ya Newcastal Utd ambapo Huddersfield wameibuka na ushindi wa bao 1-0 kupitia kwa Aaron Mooy dk 50.

No comments