Wayne Rooney astaafu soka kwenye timu yake ya taifa ya England
Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kukataa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachomenyana katika mechi za kufuzu kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Everton aliombwa na meneja wa timu ya taifa ya England kushiriki katika mechi dhidi ya Malta na Slovakia.
”Nimetimiza ndoto yangu ya kuitumkia timu yangu ya taifa ya England kila mara nilipochaguliwa ilikuwa fahari kwangu lakini naamini kwa sasa nahitaji kupumzika”, amesema Wayne Rooney kwenye taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa habari.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United ameifungia timu ya taifa ya England magoli 53 katika mechi 119 za kimataifa tangia mwaka 2003.
No comments