Usikose Hizi Hapa

VIDEO;FIFA waamuru mechi ya Afrika Kusini vs Senegal kurudiwa.Refa afungiwa kuchezesha mechi tena.

Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limeamuru mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2018, kati ya Afrika Kusini na Senegal uliochezwa mwezi Desemba 2016, kurudiwa tena baada ya refa aliyechezesha mechi hiyo kupigwa marufuku na Shirikisho hilo.
Joseph Lamptey
Mwamuzi, Joseph Lamptey raia wa Ghana, alipigwa marufuku kwa kusimia vibaya mechi hiyo ambayo iliisha kwa Bafana Bafana kuwatwanga Senegal goli 2-1.
Mwamuzi huyo aliwapa penati ya wazi Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka jana kwa kunawa mpira lakini kanda ya video baaadae ilionesha kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa Senegal, Kalidou Koulibaly.
Senegal na Afrika Kusini kwa sasa zipo kwenye nafasi ya tatu na ya nne katika kundi D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde, ambapo timu moja ya juu ndiyo itakayofuzu kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia, mwakani 2018 nchini Urusi.
Lamptey alipigwa marufuku ya maisha mwezi Machi lakini jana Jumatano marufuku hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo, Tazama video ya penati ya utata iliyomtimua refa huyo hapa chini.

No comments