CHUPA LA FRESH REMIX LINAKUJA – FID Q
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q amesema video ya ngoma yake ‘Fresh Remix’ ipo mbioni kutoka.
Katika ngoma hiyo ambayo amewashirikisha Diamond na Rayvanny ameeleza kuwa imeshakamilika licha ya kupitia upinzani mkali kutokana na verse ya Diamond katika ngoma hiyo ambayo ilisemekana ilimlenga Alikiba.
“Tumerudi katika mtari bado maisha yanaendelea kama kawaida na hivi ninavyowaambia chupa la Fresh Femix linakuja,” amesema Fid Q.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa anatambua mashabiki wake wanamdai video ya ngoma ‘Ulimi Mbili’ na kueleza kuwa nayo itatoka lakini itakuwa na kitu kingine cha ziada.
No comments