ENGLAND YAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA URUSI BAADA YA KUIFUMUA SLOVENIA
Michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi imeendelea tena usiku wa kumkia leo baada ya timu kadhaa za taifa kuingia uwanjani kutafuta tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa na ya kwanza katika mchezo wa soka ikifuatiwa na klabu bingwa barani Ulaya.
Mchezaji wa taifa ya Uingereza, Harry Kane
Timu ya taifa ya Uingereza imechomoza na ushindi wa 1-0 mbele ya Slovenia kwa bao lililofungwa na nahodha wao, Harry Kane dakika za majeruhi na kuifanya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urisi.
Uingereza ambayo ilishuka katika dimba la Wembley ilihitaji pointi mbili pekee ili kupata nafasi ya kushiriki katika michuano hiyo inayojumuisha mataifa mbali mbali duniani na hatimae Kane kufunga bao hilo katika dakika ya 94 ya mchezo wa kundi F.
Na timu ya Scotland imechomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovakia bao la dakika za mwisho la Martin Skrtel limefufua matumaini ya timu hiyo kwenda kombe la dunia baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi lao.
Wakati timu ya taifa ya Ujerumani ikiwa ugenini imechomoza na ushindi wa mabaoa 3-1 mbele ya Northern Ireland.
Brazili ambayo ilishafuzu kucheza kombe la dunia imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Bolivia ambayo imeyaaga mashindano hayo huku hali ya hewa ikiwa ni tatizo hali iliyo walazimu wachezaji wa timu hiyo kutumia vifaa vya kuongeza hewa ili kurrudi katika hali ya kawaida.
Argentina ina kila dalili za kukosa michuano hiyo baada ya sare ya bila kufungana wakiwa nyumbani dhidi ya Peru.
Nahodha wake, Lionel Messi naye yuko katika mkumbo huo wa nyota wanaoweza kuikosa michuano ya Kombe la Dunia mwakani nchini Russia na litakuwa jambo baya sana kwake.
Licha ya kuwa na mchezaji bora duniani, Lionel Messi mpaka sasa timu hiyo inajumla ya pointi 25 katika michezo 17 waliyoshuka uwanjani.
Matokeo ya michezo mingine ni kama ifuatavyo.
No comments