VIDEO- BONGO MOVIE ETI NAZI INAANGUKA MWEMBENI ,MUNGU ANAWAONA; HAJI MANARA
Wasanii wa filamu Bongo, Jumanne hii wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kusambaa katika mitandao ya kijamii kipande cha video kutoka kwenye filamu kinachoonyesha tukio la nazi kuanguka mwembeni na kuua mtu.
Msemaji wa Simba, Haji Manara ndiye mtu wa kwanza kupost clips hiyo na kuandika ujumbe wa kushangazwa na tukio hilo.
“Bongo movie Sir God anawaluk mjue,,eti nazi inaanguka mwembeni!!nimeona nyingine kaka jambazi kaonja sumu!!sijui niwapige!!Shubamit @raythegreatest @wolperstylish @stevenyerere ,” aliandika Haji Manara Instagram.
Kauli hiyo iliibua hisia tofauti katika mitandao ya kijamii hasahasa kwa mashabiki wa filamu huku wengi wakionyesha kuiponda tasnia hiyo ya filamu.
Muigizaji JB na Jimmy Mafufu waliamua kumvaa Haji Manara kwa madai wameweka filamu hiyo mtandaoni bila kufanya utafiti wa kina.
“Kuhusu clip inayosambaa mitandaoni nafikiri ni kukosa maarifa na subra kwa watanzania hasa waishio mitandaoni. Clip inaonyesha nazi ikitoka juu ya mwembe na kumpiga mtu kichwa na kufa mwenzake anakimbia, nawashangaa sana watu kuiponda hiyo clip bila utafiti najiuliza mtu mwenye weledi anawezaje kuiponda movie kwa clip moja? Nawaza tu nani anayeijua theme ya hadithi hiyo? Je nani anajua yule binti alikimbilia wapi labda alikwenda kutoa taarifa kijijini kuwa “Ni ajabu na kweli Nazi imedondoka juu ya Mwembe na kumuua Mtu kisha tukio hilo likageuka kuwa falsafa ya mtunzi na hadithi kuhamia katika tukio hilo?” alikomenti JB kwenye video hiyo.
Aliongeza,”Lakini nani anajua kuwa pengine hiyo ni Filamu ya kichawi ambapo mchawi hashindwi kuangusha Nazi juu ya Mwembe ili kudhihirisha uchawi wake? Binafsi nazidi kuona upeo Mdogo wa Raia wengi wanaotumia Mitandao ya kijamii most of them ni waropokaji hupenda kuitumia mitandao kuharibu maisha na kazi za watu wengine kwa makusudi na ndio hao ukifanya kitu kizuri hauwaoni kupongeza Bali hujitokeza ukiharibu,”
“Mwisho kama filamu hiyo haitaendana na mawazo yangu niliyoyafikiri kabla ya kuwahukumu hakika muandaaji atakuwa ni mpuuzi wa karne na hafai kuwa sehemu ya Tasnia ya Filamu lakini kama Filamu hiyo itaenda sawa na mawazo yangu basi wapuuzi watakuwa ni wale walioiponda bila utafiti. Ni vema watumiaji wa mitandao tujifufunze kutafiti mambo kabla hatujawalisha walaji maana vinginevyo tunakuwa sehemu ya kuiposha jamii yetu”
No comments