Usikose Hizi Hapa

MPANGO WA NYUKLIA WA IRAN: TRUMP ATARAJIA KUJIONDOA

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutounga mkono makubaliano ya kinyuklia na Iran Ijumaa na kuweka chini mkakati wa kukabiliana na mpango huo.
Waandamanaji nje ya Ikulu ya Whitehouse wamemtaka rais Trump kuunga mkono makubaliano hayo.
Hatua hiyo hautaiondoa Marekani katika makubaliano hayo lakini utalipatia uwezo bunge la Congress siku 60 kuamua iwapo itafanya hivyo kwa kuiwekea Iran Vikwazo.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson amekuwa akijadiliana na wenzake kutoka Ulaya na China kulingana na maafisa.
Bwana Trump amekuwaa akishinikizwa nyumbani na ughaibuni kutofutilia mbali mpango huo.
Chini ya makubaliano hayo ya 2015 , Iran ilikubali kusitisha mpango wake wa kinyuklia kwa lengo la kuondolewa kwa muda baadhi ya vikwazo ilivyowekewa.
Rais Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani
Rais Trump amekuwa mkoasoaji mkubwa wa makubaliano hayo na akaahidi kuufutilia mbali wakati wa kampeni.
Bunge la Congress litamtaka rais kuthibitisha kila siku 90 kwamba Iran inatekeleza makubaliano hayo.
Rais Trump tayari amethibitisha mara mbili .
Uvumi kwamba rais Trump huenda akakataa kuthibitisha kwamba Iran inatekeleza makubaliano hayo umezua hofu miongoni mwa washirika wa Marekani pamoja na maafisa wa utawala wake.
Waziri wa Ulinzi James Mattis aliambia kikao cha bunge la Seneti mapema mwezi huu kwamba sio lengo la taifa la Marekani kusita kuunga mkono mkataba huo.
Rais Trump ameutaja mkataba huo kuwa mbaya zaidi na kuonya kuufutilia mbali.
>>>>>>CHANZO BBC<<<<<<

No comments