Usikose Hizi Hapa

MTUMBWI WAZAMA NA KUUA WATU WATATU ZIWA VICTORIA

Watu watatu wamekufa maji  ndani ya Ziwa Victoria katika Kisiwa cha  Ilamba wilayani Muleba baada ya mtumbwi kuzama.
Watu hao walikuwa wakitoka kuchota maji Kisiwa cha Mazinga. Mwili mmoja umeshaopolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema watu hao walizama  Jumatatu saa 6:30 mchana.

Amesema miili ambayo haijapatikana ni ya Superius Severine (27) mkazi wa Kijiji cha  Nyakitaba na Evelius Zephrine (22) wa Mubunda Kitoko wilayani Muleba


Kamanda Olomi amesema mwili uliopatikana ni wa Adela Andrea (26),  mkazi wa Kijiji cha Itongo.

Amesema Nelson Boniphace (20), mkazi wa Kisiwa cha Ilamba aliogelea na kuokolewa.

Mtumbwi huo uliokuwa na madumu 33 ya maji amesema unamilikiwa na Rashidi Sabini (33), mkazi wa Kijiji cha Ilamba.

Amesema mtumbwi huo kutokana na upepo ulipigwa na wimbi hivyo ulipinduka na kuzama.

No comments