MESSI AIPELEKA ARGENTINA KOMBE LA DUNIA KWA KUICHAPA HAT TRICK ECUADOR
Lionel Messi alifunga mabao matatu na kuiwezesha Argentina kutoka nyuma ugenini dhidi ya Ecuador na kuwalaza 3-1 na kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Brazil walikuwa tayari wamefuzu.
Luis Suarez alifunga mabao mawili kuwawezesha Uruguay kulaza Bolivia 4-2 na kufuzu pia.
Colombia pia wamesonga mbele baada ya kutoka sare 1-1 ugenini Peru.
Peru walimaliza wa tano katika michuano ya kufuzu Amerika Kusini na sasa watakutana na New Zealand katika mechi mbili za muondoano za kufuzu.
Lakini nyota wa Arsenal Alexis Sanchez na taifa lake la Chile wako nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa 3-0 ugenini Brazil.
Argentina walianza siku wakiwa nambari sita na kwenye hatari ya kutofuzu kwa mara ya kwanza tangu 1970.
Aidha, walianza vibaya katika mechi hiyo iliyochezewa mji ulio nyanda za juu wa Quito. Wenyeji walijiweka kifua mbele baada ya sekunde 38 kupitia bao la Romario Ibarra, bao la kasi zaidi ambalo Argentina wamewahi kufungwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.
Hata hivyo, Argentina, waliomaliza wa pili Kombe la Dunia nchini Brazil 2014, walijikwamua wakisaidiwa sana na ustadi wa Messi.
Alisawazisha baada ya dakika 12 aliposhirikiana vyema na nyota wa zamani wa Manchester United Angel di Maria.
Bao lake la pili alilipata dakika nane baadaye na kisha akafunga la tatu na la ushindi kipindi cha pili.
Chile, ambao wameshinda Copa America katika michuano miwili ya karibuni zaidi, walikuwa wanapigania kufuzu kwa mara yao ya tatu mtawalia baada ya kufuzu na kufika hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014.
Walianza mechi za mwisho wakiwa nafasi ya tatu lakini walifungwa mabao mawili na Brazil katika kipindi cha dakika tatu kipindi cha pili kutoka kwa Paulinho na Gabriel Jesus.
Baada ya Peru kufunga bao la dakika ya mwisho la kusawazisha dhidi ya Colombia, Chile walihitaji kufunga kujipatia nafasi ya kucheza mechi za muondoano za kufuzu.

No comments