ALICHOKISEMA NANDY BAADA YA KUSHINDA TUZO YA AFRIMA 2017
Baada ya msanii wa muziki wa Bongo Flava, Nandy kushinda tuzo ya AFRIMA 2017 amefunguka mambo kadhaa kuhusu ushindi huo.
Muimbaji huyo ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Female Artist In Eastern Africa Award, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa isingependeza kwa wasanii wote kwenda na kurudi mikoni mitupu, hivyo ushindi huo ni kitu kikubwa sana.
“Kiukweli nimefurahi sana, namshukuru sana Mwenyenzi Mungu, mashabiki wangu, Watanzania wana nguvu sana yaani nilikuwa nahofia hawapigi kura lakini wana umoja wanahitaji tuzo irudi nyumbaji” amesema Nandy.
“Nilisema mwanzoni mimi Vanessa Mdee na Feza Kessy lazima mmoja wetu airudishe nyumbaji, tumeenda wengi tusipate aibu hatimaye imeangukia kwangu nashukuru media zote” ameongeza.
Katika tuzo hizo zilizotolea nchini Nigeria usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria, msanii mwingine kutoka Bongo aliyeshinda ni Alikiba ambaye ameshinda tuzo mbili katika vipengele vya Best Africa Collaboration na Best Artist or Group in Africa RnB and Soul.
No comments