Usikose Hizi Hapa

BEKI KISIKI WA ZAMANI WA STOKE CITY AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 25

Beki wa zamani wa klabu ya soka ya Stoke City ya Uingereza, Dionatan Teixeira amefariki dunia Jumapili hii akiwa na umri wa miaka 25.

Teixeira ambaye ni raia wa nchini Brazil alifariki kutokana na kupatwa ghafla na mshtuko wa moyo.

Kwa mujibu wa klabu yake ya FC Sheriff ya Moldovia ambayo anaichezea inayoshiriki kombe la Europa League, imethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha.
Beki huyo alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya muda mrefu wakati alipokuwa na Stoke City na alifanikiwa kuichezea mechi mbili pekee ingawa alidumu kwa takribani kwa misimu mitatu ndani ya timu hiyo.

No comments