Usikose Hizi Hapa

HALI YA SAMATTA YAENDELEA KUIMARIKA

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ameanza kuonekana akifanya mazoezi mepesimepesi ya kutembea kwa kutumia fimbo maalum.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta
Samatta kwanyakati tofauti ameonekana akiwa na fimbo zinazomsaidia kutembea huku goti lake la mguu wa kulia likionekana kufungwa bandeji.
Samatta ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti siku chache zilizopita baada ya kuumia ndani ya klabu yake hali iliyopelekea kukosa kujumuika na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) atakuwa nje ya Uwanja kwa muda wa majuma sita hii ni kwa mujibu wa daktari aliyemtibu.

No comments