Usikose Hizi Hapa

HARMONIZE KUFANYA KOLABO NA SARKODIE

Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize ameingia location kufanya video na rapper kutoka nchini Ghana, Sarkodie.
Muimbaji huyo ambaye anafanya  vizuri na ngoma ‘Shulala’ ambayo amemshirikisha Korede 
Bello kutoka Nigeria amezidi kuonyesha njaa ya kutusua kimataifa. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ame-share video fupi inayowaonyesha wakiwa location na kuandika;
Let’s connect to this east & west!!! 🇹🇿 + 🇬🇭 bro @sarkodie x #KONDEBOY🎥@sallam_sk#WCB4LIFE


Harmonize anaingia katika orodha ya wasanii kutoka Afrika Mashariki kufanya kolabo na Sarkodie baada ya Victoria Kimani kutoka nchini Kenya. Utakumbuka mapema mwezi huu Harmonize alionekana tena location akifanya video na Yemi Alade kutoka nchini Nigeria.

No comments