VIDEO;JACOB ZUMA-MUGABE YUPO CHINI YA ULINZI WA JESHI
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa amewasiliana na kiongozi mkuu wa Zimbabwe, Robert Mugabe kwa njia ya simu na kudai kuwa Rais huyo yupo salama chini ya ulinzi wa majeshi ya nchi hiyo.
Bwana, Zuma amesema amezungumza na kiongozi huyo mapema leo baada ya kupata taarifa kuwa jeshi la nchi hiyo limezingira makao makuu ya Shirika la Utangazaji nchini humo (ZBC).
Zuma amesema kwamba amewasiliana pia na Majeshi ya Ulinzi ya Zimbabwe (ZDF), ambapo amepanga kuongea na pande zote mbili huku akiwataka wananchi wa Zimbabwe kuwa watulivu.
Jacob Zuma ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC yupo katika kipindi kigumu kutafuta suluhu za mgongano wa kisiasa nchini Zimbabwe.
Tazama taarifa hiyo iliyotolewa na Rais Jacob Zuma (video by France 24)
No comments