Usikose Hizi Hapa

JAMII YAKUMBUSHWA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI UNAOATHIRI MAKUZI YAO

Jamii imeendelea kukubushwa  kumlinda mtoto na vitendo mbalimbali vya ukatili ,kwani vitendo hivyo vinaathiri makuzi na maendeleo ya mtoto.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya Dr.Neema Rusibamayila  wakati wa mkutano na wanahabari mara baada kufungua mkutano wa kimataifa uliyowakutanisha wadau mbalimba kujadili afua mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumika katika nchi mbalimbali katika kuendeleza makuzi ya mtoto.

Dr.Rusibamayila ambaye alikuwa amemwakilisha katibu Mkuu wa wizara hiyo ,amesema kuwa licha ya vitendo vya ukatili kupungua kwa kiasi kikubwa lakini jamii in apaswa kuendelea kushirikiana kumlinda mtoto na vitendo vya ukatili.
Pia amewasisitiza wazazi kupenda  kukaa na watoto wao na kuwasemesha na kucheza nao kwani hatua hiyo ni muhimu  katika makuzi ya mtoto.

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka taasisi ya maendeleo ya Kibinadamu kutoka Chuo Kikuu cha Aga khan Leonard Chumo Alex  utafiti uliyofanywa unaonesha kuwa watoto wengi ambao hawafikii malengo yao ya ukuaji hivyo kupitia mkutano huo mbao uanatarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi utasaidia kuweka mikakati ya namna ya kuwekeza katika makuzi ya mtoto katika maeneo ya Afya,Elimu na Lishe.

Mkutano huo ambao umeitishwa na shirika la kuhudumia watoto Duniani UNCEF kwa kushirikiana na shirika la afya Duniani( WHO)umewakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Taasisis ya Maendeleo ya Kibinadamu ya  Chuo Kikuu cha Aga Khan,vyuo na mashirika yasiyoyakiserikali,wawakilishi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Zambia ,Kenya na Uganda pamoja na wataalamu mbalimbali wa  afya.


No comments