Usikose Hizi Hapa

SERIKALI YAKIRI UWEPO WA CHANGAMOTO KUWAFUNDISHA WATOTO WENYE MATATIZO YA AKILI

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia, William Ole Nasha ammesema ni kweli kwamba kuna changamoto za kutosha kwaajili ya kuwafundisha watoto wenye matatizo ya akili.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia, William Ole Nasha
Akizungumza leo Bungeni Mh. Nasha amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo serikali imejipanga katika siku zijazo kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.
“Ni kweli kama alivyosema kwamba kwa kiasi fulani kuna kuwa na changamoto za kutosha kwaajili ya kuwafundisha watoto wenye matatizo ya akili na usonji nimuhakikishie tu Mh. mbunge kuwa pamoja na changamoto hiyo wizara imejipanga katika siku za huko mbele kuhakikisha hili tatizo linaondoka,” amesema Nasha.
“Mikakati hiyo imeanza kujenga chuo cha kisasa cha kufundishi walimu cha Patandi tunajenga the state of the art collage kwaajili ya kuwafundisha walimu kwaajili ya kuwafundisha walimu wenye mahitaji hayo niwahakikishie kwamba sio kwamba serikali haijajipanga.”

No comments