Usikose Hizi Hapa

SERIKALI YATOA FURSA YA MIRADI MBALIMBALI KWA WAKANDARASI WAZAWA

Serikali imekuwa ikitoa miradi maalum kwa wakandarasi wa ndani ili kuboresha maslahi yao na uchumi wa nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamuhanga wakati alipofungua mkutano wa Wakandarasi nchini na kuwatuku vyeti vya ukandarasi bora uliofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jiji Dar es Salaam.

Nyamuhanga amesema Serikali inatambua mchango wa Wakandarasi wa ndani katika kuimarisha na kuendeleza uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki cha Tanzania ya viwanda.

Amesisitiza kuwa miradi ya umeme, maji, na bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, ni fursa kwa Wakandarasi wa Tanzania kuzitumia ili kukuza weledi na utendaji wa kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakandarasi (CATA), Lawrence Mwakyambike ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapa Wakandarasi wa ndani kipaumbele katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na ufanisi.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuhakikisha wanaunga mkono swala la Rais kuhusu kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.




No comments