Usikose Hizi Hapa

MAMA WEMA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MWANAE KUTOKA CHADEMA NA KUHAMIA CCM

Mama mzazi wa msanii Wema Sepetu ambaye hapo jana ametangaza kurudi CCM, Bi, Mariam Sepetu, amesema kitendo cha Wema kurudi CCM bila kumuomba ushauri ni kitu ambacho kimemdhalilisha kama mzazi.
Mama Wema ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia kitendo cha Mawanaye kurudi CCM, huku lawama nyingi zikiwa zinamuelekea yeye kama mzazi kwa kutomshauri vema binti yake.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo, mama Wema amesema watu wanaomshauri Wema kama wazazi wake si watu wazuri akimtaja Steve Nyerere, huku akisema hawana mapenzi ya kweli na Wema kwani alipopata matatizo walimkimbia, na badala yake CHADEMA ndio waliokuwa wakihangaika naye.

"Nasema haya kuhusiana na Steve, Wema alipopata matatizo hakuweza kutokea central kumuona Wema, leo anashangilia Wema kurudi CCM, lakini akumbuke mimi nitabaki kuwa mzazi, CHADEMA walipoona nataabika nahangaika, waliweza kuja mpaka nyumbani kwangu, kuja kutoa pole, wamemsaidia Wema, napenda kusema CHADEMA ni familia moja, na nilijua kwamba kama kunalolote Wema angerudi kutaka ushauri kwangu, hiki sio kitu chepesi, ni kitu ambacho kimenidhalilisha, kimenitoa utu na najisikia vibaya", amesema mama Wema.

Pamoja na hayo mama Wema amesema Wema atabaki kuwa mtoto wake na hawezi kumchukia kwa sababu ya kuhama chama, ingawa kitendo hiko kimemuumiza.

No comments