Usikose Hizi Hapa

PICHA: MTANZANIA EMMANUEL AUSTIN ALIVYOFANYA TAMASHA LAKE LA TATU MWAKA HUU NCHINI UJERUMANI

Ndoto za Emanuel Austin kwa mwaka 2017 zimefanikiwa baada ya kukamlisha kufanya tamasha la tatu kama alivyopanga mwanzoni.
Austin ambaye ni mwalimu wa dansi (Choreographer) nchini Ujerumani akishirikiana na mkewe Larissa Bertsch, Jumamosi iliyopita wamefanya tamasha hilo katika ukumbi wa chuo chao wanachomiliki cha Tanzschule Weiss kilichopo katika mji wa Frankfurt.
Akiongea na Bongo5, mwalimu huyo wa dansi amesema katika tamasha hilo la tatu limekuwa na mafanikio makubwa zaidi pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu waliohudhuria katika tamasha hilo ambao walikuwa ni 11,000 tofauti na katika tamasha lililopita ambalo lilihudhuriwa na watu 10,000.

No comments