SHILOLE ASISITIZA KUFUNGA NDOA MWEZI HUU
Zikiwa zimesalia siku kadhaa mwaka 2017 kumalizika, msanii Shilole amezidi kusisitiza azma yake ya kufunga ndoa kwa mwaka huu ipo pale pale.
Mwishoni mwa weendend iliyomalizika katika sherehe ya ndoa ya Dj wa Clouds Media, Dj Zero shilole katika kutoa nasaha zake alisema mwezi huu atafunga ndoa.
Pia hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Shilole alimweleza msanii wa filamu Bongo, Steven Nyerere kuwa harusi yake ipo pale pale.
Shilole ambaye yupo katika mahusiano na mpenzie, Uchebe hivi karibuni walioneka wakiwa wote Igonga, Tabora nyumbani kwa kina Shilole. July Mwaka huu ndio Shilole alimuweka wazi mpenzi wake huyo na kueleza mwaka watafunga ndoa.
No comments