MRITHI WA PHILIPPE COUTINHO NDANI YA LIVERPOOL ATAJWA
Wamiliki wa klabu ya Liverpool wamepanga siku ya leo kumpatia Jurgen Klopp maamuzi yao ya mwisho kuhusu Philippe Coutinho kama ataondoka katika dirisha hili la dogo la usajili na kujiunga na Barcelona.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na gazeti la The Times zinasema kuwa Liverpool wapo tayari kupokea dau la paundi milioni 133 za usajili wa Coutinho lakini pia Klopp ana uwezo wa kuikataa ofa hiyo.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa Barcelona wameonyeshwa kukerwa na mshahara ambao Coutinho atalipwa kama atajiunga na vinara hao wa La Liga . Mshahara ambao Barca umepanga kumlipa mchezaji huyo ni takribani kiasi cha paundi milioni 10.5 kwa mwaka kwa taarifa ambazo zimetolewa na mtandao wa Hispania wa Diaro Gol.
Wakati huo huo Liverpool wameanza kumuwinda nyota wa Monaco, Thomas Lemar kwa ajili ya kuziba pengo la Coutinho endapo ataondoka na watalazimika kulipa kiasa cha paundi milioni 90 kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo.
Lemar (22) amekuwa akiwindwa na Liverpool pamoja na Arsenal kwa muda sasa lakini nyota huyo wa Ufaransa anadaiwa kuchagua kutua Anfield kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Daily Express.
No comments