Usikose Hizi Hapa

WALIOFARIKI MV NYERERE NI ZAIDI YA 100, ZOEZI LA UOKOAJI KUHITIMISHWA LEO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema uokoaji wa miili ya waliofariki dunia baada ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere utakamilika leo Septemba 21, 2018 kabla ya saa 12 jioni.

Kamwelwe ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha Taifa (TBC), akiwa eneo la tukio Kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

Mpaka sasa miili zaidi ya 100 imepatikana katika ajali hiyo kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

No comments