POGBA AWEKEWA UZIO KUSEPA MAN UTD
Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba lazima atumie nguvu msimu huu kama anampango wa kuondoka ndani ya kikosi hicho kujiunga na Real Madrid.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Manchester United, Ed Woodward amezuia madili yote ambayo yanayomhusu kiungo huyo kwa sasa.
Hata kama, Ole Gunnar Solskjaer,ana furaha kumruhusu kiungo huyo bado kuna uwekezakano wa kubaki ndani ya kikosi hicho na kama akibaki huenda asiwe na furaha.
Woodward anaamini kwamba kumuuza mchezaji ambaye ni mshindi wa kombe la Dunia kutaigharimu timu.
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane hata kama amemwambia Pogba anamhitaji kwa muda huu ama baadaye itakuwa ngumu kumpata.
No comments