Waziri Nape Kawajibu Waliobeza Diamond Platnumz Kukabidhiwa Bendera Ya Taifa.......Ridhiwan Kikwete Hajataka Kukaa Kimya, Kamjibu Tena Nape
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Tanzania Nape Nnauye sio kwamba hakuona maoni ya Watanzania kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye kumkabidhi bendera mwimbaji wa bongofleva Diamond Platnumz kwenda Gabon kwenye michuano ya Afrika.
Waziri Nape ameziona comments za Watanzania na yeye amewajibu baada ya Diamond kuhudhuria kwenda kutumbuiza kwenye mashindano hayo ya soka Afrika yanayofanyika Gabon ambapo Nape baada ya kuona imekua gumzo mitandaoni yeye kumpa Diamond bendera.
Kupitia Twitter yake Waziri Nape alichukua picha ya Diamond akiwa na wengine wa Afrika walioziwakilisha nchi zao kwenye mashindano yao wakiwa na bendera na kuandika "Ulizeni tena kwanini nilimkabidhi bendera Diamond"
==>Kwa sababu mjadala umekua mrefu sana kupitia twitter,baada ya post ya Waziri Nape kwenye watu walioandika tena ni Mbunge Ridhiwani Kikwete ambaye ameandika: Nafikiri Waziri amepanik kutokana na mashambulizi lkn ukweli ni kuwa tunahitaji kushiriki afcon 2019
No comments