Vanessa Mdee asimulia kilichotokea baada ya kupigwa chini B’Hits na alivyokutana na Nahreel
Vanessa Mdee, Gosby, Mabeste na wengine, walijikuta wakihaha miaka takriban mitatu iliyopita baada ya kupigwa chini na label ya B’Hits. Kipindi hicho Vee ndio alikuwa ameanza kupata umaarufu.
“Nilipigwa chini na label, label ilinipiga chini kama kiazi chenye moto,” Vee alisema kwenye mahojiano na kipindi cha Up Close & Personal cha K24 ya Kenya.
“Waliniacha kwa sababu ambazo zilikuwa zikijirudia, ulikuwa ni wasaa mchungu mtamu kwasababu kipindi hicho Closer ilikuwa inafanya vizuri sana, Me & You ilikuwa inafanya vizuri sana kwahiyo nilihitaji zaidi na nilikuwa nazo zaidi kwenye studio lakini tuligombana sasa ningeweza kwenda kuchukua muziki?”
Aliendelea, “Kwahiyo nikasema nahitaji kumpata mtu ambaye anaweza kupatia sauti yangu. Shout out kwa Hermy kwasababu sasa sisi ni familia, ni kaka yangu daima. Kwahiyo nilikuwa naijua hii bendi ya Navy Kenzo toka Arusha na wakati huo walikuwa wakijulikana kama Pah One. Pah One ikaja kuvunjika na wawili kati yao walikuwa wanataka kwenda nje kusoma masters, nilienda kwenye studio yao ambayo wakati huo ilikuwa nyumba yao na nikamuambia Nahreel ‘nakuaminia, nadhani mimi na wewe tunaweza kufanya mambo makubwa pamoja.’
“Muda huu Nahreel alikuwa tayari kufungasha virago na kuondoka ‘nimechoka na mambo haya ya muziki.’ Na nikamuambia, acha tufanye kazi na nikamuambia ‘nichezee nyimbo zako’ pamoja tulielewana sana na imekuwa ni story tangu hapo na ninajivunia sana Navy Kenzo na Nahreel ni genius na ndiye mtayarishaji mkuu wa album yangu.”
No comments