Usikose Hizi Hapa

G-Nako ataja mambo anayoyaangalia kabla hajashirikishwa na msanii yoyote


Rapper G-Nako ametaja kitu anachokiangalia kwa msanii ambaye anataka kufanya naye kolabo.
Hitmaker huyo wa OG, amedai kuwa vitu vikubwa anavyoviangalia kwanza ubora wa kazi anayotaka kushirikishwa na malengo ya msanii mwenyewe kwenye kazi hiyo.
“Kabla ya kufanya kolabo na msanii yeyote kwanza kitu nachozingatia sana kwanza kazi iwe nzuri halafu lazima nijue hiyo kazi tunafanya katika malengo gani. Ninajua unaweza ukafanya kazi na mtu. Watu wengine wanakuwa wazembe kufanya vitu kama promosheni, videos. Unaweza ukafanya kolabo nzuri lakini pia inaweza isifanye vizuri kwa kuwa yeye mwenyewe anakuwa hajajipanga,” amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.
Rapper huyo ni miongoni mwa wasanii wa Bongo ambao wameshirikishwa kwenye kazi nyingi.

No comments