Usikose Hizi Hapa

MAKALA BURUDANI: Hisabati za Diamond Platnumz Zinagonga Vichwa Vya Wasanii Wengine Nchini

Katika kikao cha viongozi wa Wizara ya Elimu kilichofanyika miaka ya 1964/65 walikubaliana kuanza kufundishwa kwa somo la hisabati badala ya hesabu lilokuwa ikifundishwa hapo awali na hii ni kwa nchi za Afrika Mashariki.
Hivyo basi, hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu, kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo.
Somo hili kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu wa kisayansi. Hivyo huweza hutumiwa na masomo mengine kama Physics, Geography, Chemistry nakadhalika katika mafunzo yake, tuachane na hilo.
Hisabati za Diamond
Muimbaji huyo wa Bongo Flava ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Hallelujah’ aliyowashirikisha Morgan Heritage amekuwa na hisabati ambazo pengine ni zenye kuumiza kichwa katika muziki wake.
Hesabu hizo ni za kiwango cha juu kabisa, kiwango ambacho ungeweza kuita standard gauge iwapo muziki wake ungekuwa ni reli, hata hivyo hesabu hizo huenda zikawa kwake nyepesi kwa namna anavyopeleka muziki wake ila kwa wale mashabiki wake wakaona ni kazi ngumu.
Kwa namna anavyokokotoa hisabati hizo kwa kuzingatia uweledi wa kiwango cha juu kabisa na kupatia ndivyo mashabiki wake wanazidi kupata muziki mzuri. Hatari ni kwamba kukosea kanuni/njia ya hisabati matokeo yake ni kupata jibu ambalo si sahihi hivyo utakuwa unawaboa mashabiki.
Hivyo basi kufuata kanuni/njia sahihi bila kujali mrefu au ugumu wake ni mwanzo wa matokeo/majibu sahihi. Uzuri ni kwamba Diamond analifahamu hilo katika hisabati zake za kimuziki.
Hisabati Pasua Kichwa
Diamond kwa mwaka huu ametoa nyimbo nyingi kwa mfululizo na kizuri zaidi ngoma hizo ni kali zaidi kuanzia audio hadi video, zote ni level za kimataifa.
Kwa mwaka huu alianza kwa kutoa ngoma ‘Marry Me’ ambayo alimshirikisha Ne-Yo kutoka nchini Marekani, ngoma hii ilitoka February 2 na baada ya hapo aliendelea na project nyingine kama show, matangazo na shughuli mbali mbali ndani ya label yake ya WCB.
June 21, 2017 aliamua kutoa ngoma mbili kwa wakati mmoja, ngoma hizi ni I Miss You na Fire ambayo alimshirikisha Tiwa Savage kutoka nchini Nigeria. Wakati ngoma hizi zikiendelea kufanya vizuri katika media rotation, Jul 10 aliamua kutoa ngoma ENEKA ambayo hadi sasa ipo katika chati mbali mbali za radio na tv.
Na mwisho September 28 ameachia ngoma nyingine ‘Hallelujah’ ambayo mapokezi yake yamekuwa makubwa kuliko ngoma nilizozitaja hapo awali. Hallelujah imeweza kupata views milioni moja katika mtandao wa YouTube ndani saa 15 na kijiwekea rekodi ya kipekee barani Afrika.
Hisabati inapofanya kazi: Tangu siku aliyotoa wimbo wa kwanza kwa mwaka huu ‘Marry Me’ hadi  ‘Hallelujah’ ni ndani ya siku 238 ambapo ukigawanya kwa 4 ambayo ni idadi ya nyimbo alizotoa kwa kipindi hicho unapata 59.5, kwa makadirio ni sawa na siku 60 sawa na miezi miwili.
Hivyo basi Diamond ana wastani wa kutoa wimbo kila baada ya miezi miwili kwa mujibu wa hesabu hizo ambazo huhitaji kiwango cha elimu cha PhD kuelewa, ni rahisi tu.
Hata hivyo kuenda hisabati hii ikawa zaidi ya pasua kichwa kwani kuna ngoma mbili ambazo hazipo katika idadi niliyoitaja. Ngoma hizo ni Zilipendwa iliyotoka August 25 na kuwashirikisha wasaniii wote wa WCB pamoja na ngoma ‘Love You Die’ aliyoshirikishwa na Patoranking kutoka Nigeria, ngoma hii ilitoka September Mosi mwaka huu.
Hivyo idadi ngoma alizotoa ndani ya siku 238 ni 6,  ukichukua namba ya awali na kugawa kwa sita unapata 39.6. Kwa hiyo Diamond anakuwa na wastani wa kutoa wimbo kila baada ya siku 40 tukilileta jibu letu katika makadirio ambayo ni sawa na mwezi mmoja na siku 10 kitu ambacho si rahisi kwa wasanii wengi. Naomba kuwasilisha.
COPYRIGHTED BY BONGO 5

No comments