Usikose Hizi Hapa

Picha: Hii ndio jezi mpya itayotumiwa na Everton Tanzania

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imetangaza jezi mpya ambazo watakuwa wakizitumia katika michezo yao ya nje.


Rooney akiwa kwenye jezi mpya
Everton ambayo ilishika nafasi ya sita katika msimu wa 2016/2017, huwenda ikavaa jezi hizo mpya katika mechi yao ya kesho kutwa dhidi ya Gor Mahia.
Gor Mahia wanawasili nchini Tanzania Jumanne hii huku ratiba ya Everton kuwasili ilikiwa bado haijawekwa wazi.
 Tayari homa ya mpambano huo miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa huku wengi wakiwa na shauku ya kuwaonya nyota mbalimbali wa Everton kama vile Jordan Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.
Viingilio vya mchezo huo ni Sh 8000/= kwa VIP C na Sh 3000/= kwa viti vya mzunguko na mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni.

No comments