GRIEZMANN ASAINI MKATABA MPYA MNONO ATLETICO MADRID
MSHAMBULIAJI Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Atletico Madrid hadi mwaka 2022.
Lakini Mfaransa huyo amepinga klabu hiyo kupandisha dau lake na sasa itaigharimu Manchester United Pauni Milioni 88 ile ile kama ada ya uhamisho iwapo itahitaji tena kumchukua mchezaji huyo mwaka ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameingia pia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sasa akipoka Pauni 235,000 taslimu kwa wiki sawa na Pauni Milioni 12.3 kwa mwaka.
Hiyo ni pungufu kidogo kutoka mshahara wa Pauni 300,000 ambao inafahamika Man United ilimuandalia. Lakini dili hilo linamfanya awe mchezaji anayelipwa zaisi Atletico Madrid na katika La Liga sasa anazidiwa na Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar kwa mshahara mkubwa.
Atletico Madrid imelazimika kumpa ofa nzuri mchezaji huyo ili abaki baada ya kufungiwa kusajili na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hadi mwaka 2018.
No comments