RONALDO NDIYE MWANAMICHEZO NAMBA MOJA TAJIRI DUNIANI
PAMOJA na kuwa Mwanasokoa namba moja asiyepingika duniani, Mreno Cristiano Ronaldo pia ndiye mwanamichezo anayeingiza fedha nyingi zaidi duniani.
Jarida la Forbes limetoa orodha ya watu maarufu 100 wanaoingiza fedha nyingi na nyota huyo wa Real Madrid na Portugal anashika nafasi ya tano
Ronaldo ameporomoka kwa nafasi moja kutoka ya nne mwaka 2017, lakini mvaa jezi namba 7 huyo anaingiza Pauni Milioni 73.2 kwa mwaka.
Pato la mshambuliaji huyo lilipanda zaidi baada ya kusaini mkataba mpya Novemba mwaka jana Real Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amesaini mkataba ambao analipwa Pauni 365,000 kwa wiki Uwanja wa Santiago Bernabeu hadi mwaka 2021.
Mbali na hiyo, Ronaldo ana mkataba binafsi na Nike wenye thamani ya Pauni Milioni 790 wakati kampuni yake ya CR7 nayo inazidi kukua.
Ronaldo anatarajiwa kushinda Ballon d'Or ya tano mwaka huu baada ya kuiongoza Real kutwaa taji la kwanza la La Liga tangu mwaka 2012 pamoja na taji la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili mfululio mapema mwezi huu.
LeBron James ni mwanamichezo mwingine pekee ambaye yumo kwenye orodha huyo Pamoja na rapa Sean 'Diddy' Combs (Pauni Milioni 102).
No comments