Video: Kwaheri Bongo Fleva – Seline
Msanii wa kike Seline ambaye pia aliwahi kuwa chini ya usimamizi wa lebo ya The Industry, amefunguka sababu ya kuingia kufanya muziki wa aina ya gospel, lakini pia amedai hatafanya tena muziki wa Bongo Fleva.
Akiongea na Bongo5, muimbaji huyo amesema, “Gospel yangu mimi haitakuwa inamlenga mkristo tu, ndio maana nime-stick na kusema Mungu tu, Mungu ni wa waislamu na wakristo, kwa hiyo sitakuwa na matabaka ya kuangalia ni dini gani nina focus. Niliamua tu maana inafika point katika maisha unasema for me I have done everything, nimeimba Bongo Fleva, nimekunywa I ‘ve done everything in my life.”
Seline ameeleza kama atafanya muziki huo wa gospel moja kwa moja au atakuwa akichanganya na Bongo Fleva. “Nitafanya inspiration na gospel, but not Bongo Fleva anymore,” amesema msanii huyo.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa, hakuwahi kufikiria kufanya muziki wa injili katika maisha yake kwa kuwa kufanya muziki huo aliamini ni wito.
“Haikuwa kwenye plan, na nakumbuka walikuwa wakiniambiaga nyumbani, unaimba injili? Sina wito ni mimi that not for me, I rather not do it. Hauamki na kusema unaswitch, ilikuwa ngumu kwangu na mara ya kwanza nilikuwa nafikiri gospel ni yakina Rose Muhando. I prayed it, nikamuomba Mungu kama gospel ni yangu nionyeshe njia iliyo sahihi,” ameeleza msanii huyo.
No comments