Balozi Bethuel Kiplagat afariki dunia Kenya
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Haki na Maridhiano nchini Kenya (TJRC), Balozi Bethuel Kiplagat amefariki dunia akiwa na miaka 81.
Kiongozi huyo anadaiwa kufariki leo katika hospitali ya mjini Nairobi alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi aliyokuwa akiugua muda mrefu.
Kiplagat aliwahi kuwa mwanadiplomasia na mmoja wa viongozi wa serikali ya Kenya, ambaye alikaa kwenye kiti cha uenyekiti wa TJRC kuanzia 2009 hadi Novemba 2010 ambapo alijiuzulu baada ya kuchunguzwa kwa madai ya unyanyasaji wa haki za binaadamu hasa katika mauaji ya Wagalla ya mwaka 2004.
Wakati huo huo marehemu aliwahi kuwa balozi wa Kenya nchini Ufaransa wakati wa uongozi wa rais Moi kuanzia mwaka 1978 mpaka 1991.
No comments