Filamu ya ‘The Inner Struggle’ ukombozi wa watu wenye albinism TZ
Mwanaharaki wa kutetea haki za binadamu kutoka nchini Sweden Eva Stenbom kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Under the Same Sun (UTSS), wameandaa filamu maalum itakayotoa elimu na kuondoa dhana potofu iliyopo kwa watanzania na watu wengine kwa ujumla juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinisim).
Filamu hiyo inalenga kuondoka dhana hiyo potofu hasa ya kunyanyapaliwa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi na kuielimisha jamii ili iweze kuwaona watu hao ni watu wa kawaida kama walivyo wengine.
Filamu hiyo inalenga kuondoka dhana hiyo potofu hasa ya kunyanyapaliwa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi na kuielimisha jamii ili iweze kuwaona watu hao ni watu wa kawaida kama walivyo wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Stenbom alisema filamu hiyo itaanza kuonyeshwa rasmi Julai 15 mwaka huu kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi huko Zanzibar (ZIFF).
Stenbom ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu hiyo, alisema wameamua kuandaa filamu hiyo ijulikanayo kwa jina la The Inner Struggle baada ya kufanya utafiti na kubaini kuwa idadi kubwa ya watanzania hawawaelewi watu wenye ulemavu huo wa ngozi hali inayopelekea wanawanyanyapaa.
“Miezi miwili iliyopita nilipata taarifa kuwa ZIFF wamekubali kuonyesha filamu yangu hivyo naamini kuwa watanzania wengi na watu wengine duniani kupitia tamasha hilo wataweza kuona tulichokiandaa na wataelimika natambua kuwa tamasha hili ni kubwa sana.
“Filamu hii ina stori ya kweli na imegusa maisha halisi ya mtu hivyo itatumika kuwaeleza na kuwafumbua watu juu ya kuwaona albinisim ni watu wa kawaida kwani wana hisia mbalimbali hata maumivu wakikosewa kama ilivyo kwa watu wengine,” alisema
Aidha alisema watu hao wenye ulemavu wa ngozi wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya kuitunza ngozi yao na kujilinda wenyewe.
“Bado watu hawa hawana elimu yoyote juu ya kuitunza ngozi zao wengi wao wamekuwa wakiaribika na jua hivyo kunahaja ya kuendelea kutoa elimu na kupitia filamu ya The Inner Struggle watapata elimu hiyo,”alisema.
No comments