Usikose Hizi Hapa

ASKOFU AMPONGEZA MAGUFULI SEKTA YA MADINI...AIOMBEA MVUA ISILETE MADHARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amekuwa katika msitari wa mbele katika kusimamia rasilimali za nchi hasa katika sekta ya Madini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Good News For All Ministry Askofu Dr Charles Gadi jijini Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akifungua maombi kwa ajili ya kuombea maafa yasitokee katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini.

Amesema ni habari ya kufurahisha kwa Rais huyo kurejesha malimbikizo ya kodi ambayo kwa namna moja ama nyingine huenda Serikali isingezipata fedha hizo kama sio msimamo wake kudhibiti makampuni ya madini yanayowekeza nchini.

"tunaamini hata kwenye vito vya thamani kama almasi,tanzanite na mengineyo,kuna mengi tutafaidika nayo kutokana na usimamizi makini ambao ameanza kuuweka kwenye makampuni na machimbo husika"

Sambamba na pongezi hizo Mwenyekiti huyo ameipongeza idara ya hali ya hewa kwa kuwahi kutoa tahadhali ya kuwepo kwa mvua kubwa inayotegemewa kuleta madhara kama itanyesha kwa kiwango kilichotabiriwa.

"kwanza hii ni hatua kubwa na ya maendeleo ya kiteknolojia kwa idara yetu hiyo,jambo litakalowezesha wale walioko kwenye maeneo hatarishi kuweza kuchukua tahadhari mapema ili kulinda maisha na mali zao" amesema Dr Charles.

Aidha ameongeza kuwa wao kama Viongozi wa Dini wamekuwa katika msitari wa mbele kufanya mikutano ya kuiombea mvua kila mara kunapokuwa na uwezekano wa uhaba wa mvua nchini kwa kuwa mvua hizo ni muhimu katika kilimo cha mazao na shughuli nyingi za binadamu na Mungu amekuwa akijibu maombi yao.













No comments