Usikose Hizi Hapa

UEFA KUMSHUSHIA RUNGU PATRICE EVRA NOVEMBA 10

Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limemfungulia mashitaka ya kinidhamu beki wa klabu ya Marseille, Patrice Evra kwa kosa la kumpiga shabiki wa timu hiyo.

Evra ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Manchester United alizawadiwa kadi nyekundu kabla hata ya kuingia Uwanjani baada ya kumpiga shabiki aliyekuwa akimtupia mmaneno ya kumdhihaki.
UEFA imesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, atakosa mchezo mmoja wakati bodi inayosimamia nidhamu za wachezaji ikielekea kujadili swala hilo katika mkutano ujao Novemba 10.
Kwa upande wa klabu ya Olympique de Marseille imetoa taarifa kuwa inaendelea na uchunguzi juu ya tukio lililo tokea kati ya shabiki huyo na mchezaji Patrice Evra ambaye alikuwa akipasha misuli kujiandaa kuingia katika mchezo huo siku ya Alhamisi.
Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo wachambuzi wa soka wamelifananisha na lile alilowahi kufanya mchezaji, Eric Cantona ambaye alimpiga teke shabiki wa Crystal Palace huko Selhurst Park mwezi Januari mwaka 1995.
Mchezaji, Eric Cantona akimpiga teke shabiki wa Crystal Palace huko Selhurst Park mwezi Januari mwaka 1995.
Kufuatia tukio hilo Cantona alihadhibiwa na chama cha soka cha Uingereza kuwa nje ya Uwanja kwa miezi tisa.

No comments