Manchester United yathibitisha kumsaini Romelu Lukaku
Klabu ya Manchester United imemaliza tetesi ambazo zilikuwa zikiandikwa sana kuhusu Romelu Lukaku ambaye alikuwa haeleweki wapia atacheza msimu ujao.
Ijumaa hii ziliibuka tetesi za Lukaku kwenda Manchester United lakini baadaye tetesi hizo zikatiliwa mashaka kwani baadhi ya vyombo vya habari vilikanusha.
Usiku wa Jumamosi taarifa mpya zikaja kwamba Chelsea wanataka kuharibu dili la United kumnunua Lukaku kwa dau sawa na ambalo United wamelipeleka Everton.
Lakini leo Mnachester United wamemaliza utata wa kuhusu Lukaku baada ya klabu hiyo kuthibitisha kwamba wametuma dau kwa Everton kumnunua Lukaku.
#MUFC is delighted to announce a fee has been agreed with Everton for the transfer of Romelu Lukaku, subject to a medical & personal terms. pic.twitter.com/O7oQJWzYHo— Manchester United (@ManUtd) July 8, 2017
Katika taarifa hiyo inasema “tunafuraha kuwajulisha kwamba Everton wamekubali dau letu kwa Lukaku na sasa kilichobaki ni vipimo vya afya tu” iliandika taarifa hiyo.
Sasa kilichobaki kwa Manchestet United ni mchakato wa vipimo vya afya tu na makubaliano binafsi kuhusu mchezaji huyo ili aanze kuitumikia United.
No comments