Ipo nafasi kubwa ya Neymar kuondoka Barca na nafasi yake kuchukuliwa na Coutinho wa Liver
Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania inampango wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazili, Philippe Coutinho.
Mchezaji wa Liverpool, Philippe Coutinho
Barcelona inataka kumsajili Coutinho mwenye umri wa miaka 25, ili kuchukua nafasi ya Neymar ambaye ana asilimia 90 za kuondoka na kujiunga na matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain kwa usajili utakao weka rekodi ya dunia.
Liverpool inahitaji dau la pauni milioni 72 ili kumuachia mchezaji huyo ambaye amefunga jumla ya magoli 13 na kutoa pasi 31 zilizochangia upatikanaji wa magoli.
No comments