RAYOL SPORTS YA RWANDA KUCHEZA NA SIMBA KATIKA MAADHIMISHO YA SIMBA DAY
Kikosi cha Rayon Sports cha Rwanda ndicho kitakachocheza na Simba katika mechi ya Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kawaida tamasha hilo hufanyika Agosti 8. Rayon imekubali kushiriki tamasha hilo maarufu la Simba Day ambalo hufanyika mara moja kila mwaka.
Nchini Rwanda, Rayon ndiyo timu yenye mashabiki wengi zaidi ikifuatiwa na APR ambayo inamilikiwa na jeshi.
No comments