Kamati ya Nidhamu yamwachia huru mwingine aliyefungiwa na TFF
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF, imeendelea kuwatoa kifungoni wadau mbalimbali ambao waliokuwa wamefungiwa kutojihusisha na soka.
Damas Ndumbaro ambaye ni wakili na wakala wa wachezaji ambaye miaka mitatu iliyopita alifungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka saba ameachiwa huru.
Ndumbaro ni mtu wa pili kuachiwa na kamati hiyo baada ya hapo juzi mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kuachiwa huru kutoka kwenye kifungo alichopewa cha kutojihusisha na soka kwa kipindi cha mwaka mmoja.
No comments