PICHA/VIDEO;Majeruhi wa Lucky Vicent walikuwa hawakumbuki kilichotokea – Mh. Nyalandu (+video)
Mbunge wa Singida Kaskazini, Mh. Lazaro Nyalandu amesema kuwa wanafunzi majeruhi wa Lucky Vicent waliopelekwa nchini Marekani kwaajili ya matibabu walikuwa hawajui kilichotokea kilichokea katika ajali.
Hayo yamebainishwa na Mhe. Nyalandu ambapo alisema wataalam wa Psychologia walikaa wakafanya kikao ili kuwaambia kilichowasibu ni nini.
“Wataalamu wanaohusika na mambo ya Psychologia walikaa wakafanya kikao walipofika America kwamba hawa watoto wanaambiwa kilichowasibu nini kwasababu walikuwa hawakumbuki kilichotokea wanajua tu kuna kitu kilitokea lakini kwa kweli waliamua kuja kuwaambia namna bora ya kumfanya mtoto apone ni kumwambia kilichotokea, kwahiyo waliambiwa ndio wao watatu walipona wenzao 35 walifariki mwalimu wao alifariki dereva wao na watoto 32 na walikuwa wanauliza rafiki angu fulani, rafiki angu fulani, lakini Mungu anajua kwanini sote ni wazima,” alisema Mh. Nyalandu.
Tazama video hii:
No comments