Lewis Hamilton aweka rekodi British Grand Prix
Dereva wa magari ya Mercedes, Lewis Hamilton amefanikiwa kuweka rekodi ya kutwaa taji la mashindano ya British Grand Prix kwa mara ya tano.
Ushindi huo wa Hamilton unamfanya kuwa mshindi wa muda wote wa michuano hiyo ya magari ya British Grand Prix katika tasnia yake.
Ushindi huo wa Hamilton unamfanya kuwa mshindi wa muda wote wa michuano hiyo ya magari ya British Grand Prix katika tasnia yake.
Kwa ushindi wa Hamilton unazidi kuchochea ushindani baina yake na dereva wa magari ya Ferrari, Sebastian Vettel. Mara baada ya ushindi huo dereva huyo maarufu wa magari ya kampuni ya Mercedes amesema amefurahishwa na mchango mkubwa ulioonyeshwa na mashabiki.
“Mmenionyesha mchango mkubwa wiki hii, najivunia kwa hilo na nimefanya hili kwa sababu yenu wote. Ushindi wa British GP ni majibu tosha kwa wale waliokuwa wanatukosoa Mercedes. Kama ulikuwa ufahamu maandalizi yangu sasa utakuwa umefahamu.”
No comments