Mhe. Lowassa kuwania nafasi ya Urais
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema licha ya changamoto nyingi anazokutana nazo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), atagombea tena urais mwaka 2020.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa Nation Media Group jijini Nairobi.
“Kwa mapenzi ya Mungu nitajaribu tena mwaka 2020 na nitapita kwa mikono safi. Wafuasi wangu walitaka tuingie mitaani kudai ushindi, lakini kulikuwa na bunduki nyingi mikononi mwa wanajeshi. Niliogopeshwa na umwagikaji wa damu. Sikutaka kuingia Ikulu kupitia damu za watu kwa sababu sistahili hivyo,” alisema Lowassa.
Hata hivyo Mhe. Lowassa alisema licha ya uchaguzi uliopita kutoaminika, bado anamheshimu Dkt John Pombe Magufuli kama Rais.
No comments