Usikose Hizi Hapa

Video: Diva atia neno penzi la Ben Pol na Ebitoke

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva amezungumzia uhusiano wa msanii wa Bongo Flava, Ben Pol na mchekeshaji Ebitoke, huku akidai haijui ngoma mpya ya msanii huyo ‘Tatu’.


Mrembo huyo ameiambia Bongo5 kwanza hamfahamu Ebitoke na kama wanafanya uhusiano wao kama kiki kama alivyoelezwa na baadhi ya rafiki zake, siyo vizuri.
“Kiukweli mimi nasikia tu, simjui huyo dada kwa hiyo nikasema nataka nimtafute yule dada na Ben Pol tuone kama kweli wapo serious lakini pia nasikia wengine wanasema yule dada amelipwa, kwa hiyo mtu unalipwa anafanya vile unawaaminisha watu, kama amefanya hivyo ni kind of crazy,” amesema Diva.
Kuhusu wimbo wa Tatu wa Ben Pon, Diva amesema, “sijasikia kweli ule wimbo, nilisikia kweli Barakah kasema ni mbaya, so nikamtafuta kweli Ben Pol kwa sababu kipindi anatoa ule wimbo ndio picha zake zilianza ku-trend, so nikamtafuta nikafanya nae interview lakini nilikuwa sijasikia wimbo na hadi leo sijausikiliza wimbo wake,” amesisitiza.

No comments