Watu nane wafariki katika mafuriko Marekani
Mafuriko yaliyosabishwa na mvua kubwa katika jimbo la Arizona nchini Marekani yameua watu wapatao nane.
Mafuriko hayo yametokea maeneo ya Cold Springs karibu na Patson siku ya Jumamosi, inadaiwa kuwa kundi la watu walikuwa wamekaa karibu na mto wakifanya sherehe ndio waliopata madhara makubwa na kati ya watu nane watoto wawili wanadaiwa kufa maji.
Afisa wa Polisi David Horning ameeleza bado wanaendela na uokoaji na mpaka sasa watu nne waliokolewa wanapatiwa matibabu. Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza kuwa kutokea mvua kubwa pamoja na radi katika maeneo hayo.
No comments