Madrid kuvunja rekodi ya dunia
Klabu ya Real Madrid imeibua upya suala la usajili wa mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe baada ya kusema imekubali kumnunua mchezaji huyo kwa dau la Pauni milioni 161, lakini itamuacha kwa mkopo klabuni kwake kwa msimu mmoja zaidi.
Mchezaji wa klabu ya Monaco, Kylian Mbappe
Suala la Mbappe limeibuka leo Jumanne baada ya kimya cha muda mrefu kutokana na uongozi wa klabu hiyo kuzima purukushani za kumsajili mchezaji huyo walipotangaza kuwa hawana mpango wa kumuuza.
Real Madrid imeamua kumrudia Mbappe baada ya kumuuza mchezaji wake, Alvaro Morata. Sasa suala la Mbappe imelivalia njuga.
Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa mchezaji huyo atakuwa akipokea mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki.
No comments