USAJILI: Mbeya City yasajili mchezaji wa Ashanti
Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya imekamilisha usajili wa mchezaji, Idd Seleman kwa mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji, Idd Seleman
Nyota huyo wa zamani wa Ashanti United, anaungana na wachezaji wengine kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15, mwaka huu na litarajia kufungwa Agosti 6, huku klabu mbali mbali zikiendelea na usajili.
No comments