Mayanja-Michezo yetu ya kirafiki tutacheza nchini Afrika Kusini
Kikosi cha Simba SC ambacho kimepiga kambi nchini Afrika Kusini kwaajili ya maandalizi ya ligi kuu pamoja na michuano ya kimatifa wiki hii kinatarajia kuanza kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.
Kikosi cha timu ya Simba kikiwa nchini Afrika Kusini
Simba inatarajia kurejea nchini Agosti 6, mwaka huu kabla ya kufanyika kwa tamasha lao la Simba Day litakalofanyika Agosti 8, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Akizungumza kutoka Afrika Kusini, kocha msaidizi wa benchi la ufundi la Msimbazi, Jackson Mayanja amesema baada ya kufanya mazoezi ya nguvu kwa wiki nzima, wanatarajia wiki hii kuanza kucheza mechi za kirafiki bila ya kufafanua timu watakazocheza nazo.
“Wiki ijayo (wiki hii) ndiyo tunatarajia kuanza kucheza mechi za kirafiki, mpaka sasa bado sijafahamu ni dhidi ya timu gani tutakazocheza nazo, lakini mipango ipo hivyo.
“Kikubwa ambacho naweza kusema, mazoezi yetu yanakwenda vizuri tukiwa na wachezaji wachache ambao hawakuwa na majukumu na timu zao za taifa, lakini muda wowote kuanzia sasa tunaweza kuwapokea wale waliokuwa Taifa Stars pamoja na wachezaji wapya,” alisema Mayanja
No comments