Video: Serikali yakanusha kuingilia uchaguzi wa Kenya
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Augustine Mahiga amekanusha taarifa zinazosambaa kupitia mitandao ya kijamii na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa Tanzania inaingilia uchaguzi wa nchini Kenya kwa kuweka mitambo ya kuhesabia kura katika wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
PICHA/VIDEO kutoka BONGO 5
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Waziri Mahiga amekanusha tuhuma hizo kwa Tanzania na kueleza kuwa Tanzania haijawahi kuingilia masuala ya kisiasa hususani ya uchaguzi na haitothubutu kufanya hivyo.
Waziri Mahiga amefafanua kuwa taarifa hizi zinazushwa na wabunge wa upinzani wa Kenya na viongozi wa upinzani wa nchini Tanzania, ambapo amesisitiza kuwa serikali itachukua hatua kwa wale wote wanasambaza taarifa hizo zisizo kuwa na dhamira njema ya urafiki katika ya Tanzania na nchi ya jirani ya Kenya.
Zikiwa zimebaki wiki mbili kufanyika kwa uchaguzi wa nchini Kenya Waziri Mahiga amewatakia kila la heri wakenya katika uchaguzi wao.
No comments