Mbunge aliyesema “Kosa mwanamke kukataa tendo la ndoa” atengwa jimboni kwake
Baada ya kauli ya Mbunge mwenye ushawishi mkubwa nchini Malaysia, Che Mohamad Zulkifly Jusoh ya kupendekeza mswada bungeni kuwa wanawake watakaokataa kufanya tendo la ndoa au kukataa ndoa za mitala wachukuliwe hatua kama makosa mengine, Mbunge huyo amejikuta kwenye hali mbaya ya usalama kutoka kwenye makundi ya wanawake wanaharakati wakiandamana jimboni kwake huku wakiapa kutompigia kura mwakani.
Che Mohamad Zulkifly Jusoh
Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 58 kutoka jimbo la Terengganu, alisema kuwa wanaume wanapitia kwa asilimia kubwa wanapitia manyanyaso ya kijinsia na kuharibiwa kisaikolojia hasa pale wanapokataliwa kupata haki yao ya tendo la ndoa kutoka kwa wake zao.
“Licha ya wanaume kuwa wenye nguvu kuliko wanawake, wanawake huwadhulumu katika masuala kama haya kwa njia iliyo ya kuumiza, ni vema suala hili tukalifikirie likawa muswada”,amesema Jusoh wiki iliyopita kwenye vikao vya Bunge kauli ambayo imeibua taswira tofauti kwa wanawake nchini Malaysia.
Wabunge wanaume na makundi ya wanaharakati yana matumaini kuwa mswaada mpya utawakinga zaidi waadhiriwa wa dhuluma ya tendo la ndoa.
“Tumemsikia akipendekeza sheria kandamizi dhidi yetu hatukubali kukandamizwa, kwa nguvu yetu tutajitahidi kwa nguvu zetu tuweze kumshusha na tutaweza, tutamziba mdomo mwakani”,alisema kiongozi wa wanawake walioandamana jimboni Terengganu siku ya jana wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Aljaazera.
Nchini Malaysia kuna ongezeko kubwa la vitendo vya wanawake kuwanyima ujumba waume zao kitu ambacho kimekosa sheria ya kuwabana wanawake wanaofanya vitendo hivyo.
Malaysia ni nchi yenye Waisilamu wengi kwa mwanaume kuoa hadi wake wanne ikiwa watapata idhini kutoka kwa mahakama za sheria anaruhusiwa.
No comments