Baada ya Edu Boy kuwekeza milioni sita kwenye video
Msanii wa Bongo Flava, Edu Boy amedai sh. milioni sita alizowekeza katika video yake ‘Naiee’ aliyomshirikisha Bill Nass zimerejea.
Rapper huyo kutoka Rock City amesema licha ya gharama hizo kurejea lakini kikubwa alichokuwa anaangalia ni namna ya kupata connection na watu mbali mbali.
“Kikubwa zaidi niliangalia katika kupata Connection gharama sio kitu ni ubora hata ukiwa na video tatu lakini zenye ubora ambao zinaweza kukutangaza zaidi na watu kuzidi kukufahamu” Edu Boy ameiambia Bongo5.
Video hiyo aliyoongozwa na director Nisher amebainisha alimlipa sh. milioni tatu na nyingine tatu zilitumika katika gharama mbali mbali ikiwemo usafiri.
No comments